Mwaliko wa Send-off
Mpendwa Mzee Bakari na Mama
Familia ya Bw. na Bi. Bakari wana furaha kukualika kwenye harusi ya
Rehema
- Lini
- Jumamosi, 12 Desemba 2026saa 10 jioni (16:00)
- Wapi
- Mlimani City, Dar es Salaam
Karibu tusherehekee pamoja
Tengeneza kadi ya harusi, send-off, kitchen party au siku ya kuzaliwa. Itume kwa WhatsApp au SMS, pokea majibu ya wageni, na hakiki wanaoingia mlangoni kwa QR.
1Tengeneza kadi
Chagua muundo, kisha andika majina, tarehe na ukumbi. Kadi inajitengeneza mbele yako unapoandika.
2Tuma kwa wageni
Kila mgeni anapata kiungo chake binafsi kwa WhatsApp au SMS, chenye jina lake na idadi ya watu wa kadi yake.
3Pokea majibu
Wageni wanajibu kwa mguso mmoja. Unaona papo hapo idadi ya watakaohudhuria.
4Hakiki mlangoni
Siku ya sherehe, QR ya kila kadi inaskaniwa kwa simu. Kadi iliyokwisha tumika au isiyotambulika inakataliwa.
Maua ya rangi za maji kwa sherehe za upole, au pindo za kanga, kitenge na mlango wa Zanzibar kwa zenye rangi nyingi. Kila muundo unaweza kubadilishiwa rangi.
maua
Maua ya rangi za maji, kwa harusi na send-off
kanga
Pindo la kanga, kwa harusi
mlango
Mlango wa Zanzibar, kwa send-off
kitenge
Rangi za kitenge, kwa kitchen party
tingatinga
Rangi za Tingatinga, kwa siku ya kuzaliwa
mawimbi
Mawimbi ya pwani, kwa mwaliko wowote
Rekodi ahadi na malipo ya kila mchangiaji, ona salio papo hapo, na tuma vikumbusho kwa SMS kwa ambao bado hawajamaliza.
Michango ya Harusi
Imekusanywa TSh 300,000 kati ya TSh 600,000
| Mchangiaji | Ahadi | Imelipwa | Salio |
|---|---|---|---|
| Ally Hamisi | TSh 200,000 | TSh 150,000 | TSh 50,000 |
| Mama Zawadi | TSh 100,000 | TSh 100,000 | TSh 0 |
| Kaka Peter | TSh 300,000 | TSh 50,000 | TSh 250,000 |
Hapana. Kila mgeni anafungua kadi yake kwenye kivinjari cha simu kupitia kiungo alichotumiwa, kisha anajibu na kupata QR ya kuingilia hapo hapo.
Kwa WhatsApp, kila kiungo kinafunguka kwenye simu yako na ujumbe ulioandikwa tayari, bila gharama ya ziada. Kwa SMS, Kadi inatuma kwa wageni wote mara moja na unaona makadirio ya gharama kabla ya kutuma.
Ndiyo. Unaweka idadi ya watu kwa kila kadi, kwa mfano mtu mmoja, wanandoa au familia. Mlangoni kadi inaruhusu idadi hiyo tu.
Wewe au watu unaowaongeza kwenye timu kwa namba zao za simu. Wanaskani QR kwa kamera ya simu, au wanaandika namba ya kadi.
Ndiyo. Unachagua Kiswahili au Kiingereza kwa kila tukio, na kadi nzima, pamoja na muda, inaonyeshwa kwa lugha hiyo.
Karibu tusherehekee pamoja
Unahitaji namba ya simu tu. Unda tukio, ongeza wageni na uwatumie kadi siku hiyo hiyo.
Unda kadi yakoTunaweza kukubunia kadi yenye picha zenu, rangi za sherehe yenu na maneno maalum.