Sera ya faragha
Ilisasishwa mwisho Jumanne, 15 Septemba 2026
Kadi inawasaidia wenyeji kutengeneza na kutuma kadi za mwaliko za kidijitali. Sera hii inaeleza taarifa tunazokusanya, tunavyozitumia na haki zako, kwa kuzingatia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Tanzania ya mwaka 2022.
Taarifa tunazokusanya
Wenyeji na wasaidizi: jina na namba ya simu mnayotumia kuingia.
Wageni na wachangiaji: majina, namba za simu na idadi ya watu ambazo mwenyeji au kamati wanaziingiza. Majibu ya mwaliko na ujumbe ambao mgeni anaandika, kumbukumbu za kuingia mlangoni, na rekodi za ahadi na malipo ya michango.
Kumbukumbu za SMS tunazotuma. Namba za siri za kuingia hazihifadhiwi.
Kadi haipokei wala haishikilii fedha za michango, na haikusanyi taarifa za kadi za benki.
Tunavyotumia taarifa
Kukuwezesha kuingia, kuonyesha na kutuma kadi, kupokea majibu ya wageni, kuhakiki wageni mlangoni, kufuatilia michango, kutuma SMS unazoomba na kushughulikia maombi ya muundo maalum.
Kulinda huduma dhidi ya matumizi mabaya. Hatuuzi taarifa zako, na hatutumii namba za wageni kwa matangazo.
Wajibu wa mwenyeji
Mwenyeji na kamati wanawajibika kuhakikisha wana ruhusa ya kuingiza namba za simu za wageni na wachangiaji, na ya kuwatumia kadi na vikumbusho.
Tunaoshirikiana nao
Watoa huduma wanaotusaidia kuendesha Kadi: hifadhi ya data na seva (Supabase) na utumaji wa SMS (NextSMS). Wanapata taarifa zinazohitajika kwa kazi hiyo tu. Mwenyeji akituma kadi kwa WhatsApp, ujumbe unatumwa kupitia WhatsApp yake mwenyewe.
Viungo vya kadi
Kila mgeni ana kiungo chake cha kadi. Yeyote mwenye kiungo hicho anaweza kuona kadi na kujibu kwa niaba ya mgeni huyo, kwa hiyo msikitume kwa watu wasiohusika.
Muda wa kuhifadhi
Tunahifadhi taarifa za tukio hadi mwenyeji alifute. Kufuta tukio kunafuta kadi, wageni, majibu, kumbukumbu za kuingia, michango na SMS za tukio hilo. Kumbukumbu za SMS za kuingia (bila namba za siri) zinaweza kubaki kwa ajili ya usalama.
Haki zako
Unaweza kuomba kuona, kusahihisha au kufuta taarifa zako. Kama wewe ni mgeni au mchangiaji, unaweza pia kuwasiliana moja kwa moja na mwenyeji wa tukio. Una haki ya kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi.
Wasiliana nasi
Kwa maswali kuhusu taarifa zako au masharti haya, au kuomba taarifa zako zifutwe, wasiliana na timu ya Kadi.